VIDEO: Watatu watiwa mbaroni wizi wa mtandao/ Wakutwa na laini 151


Jeshi la polisi mkoani Tabora limewakamata watu  watatu kwa  tuhuma  kujihusisha na vitendo vya wizi na utapeli wa fedha kwa wananchi kwa njia ya mtandao katika maeneo tofauti ya mkoa wa Tabora, Kigoma, Singida, Shinyanga na Katavi kwa  kwa kutuma  ujumbe mfupi wa maandishi kwa wananchi wakiwataka kutuma pesa.

 Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora ACP. Emmanuel Nley amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni kutokana na msako mikali uliofanywa na askari polisi wakioongozwa  na taarifa za  kiintelijensia ambapo wezi hao wamekutwa na simu mbali mbali pamoja na laini 151 za mitandao ya simu.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE