Wanaosaka uongozi CCM kabla ya muda wapewa onyo kali


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar ndugu Tunu Juma Kondo amewatahadharisha Akina Mama wa Umoja huo kuepuka kutumiwa na baadhi ya wanachama wasiokuwa waadilifu wanaosaka nafasi za Uongozi ndani ya CCM kabla ya muda wake.

Akiwa katika ziara ya kujitambulisha kwa Kamati Tekelezaji ya UWT Wilaya ya Mfenesini huko Welezo Unguja, amesema itachukua hatua kali za kimaadili kwa mwanachama yeyote wa Umoja huo atakayebainika kutumiwa na wasaka madaraka kabla ya muda wa Kikatiba.
Amesema Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi ni waadilifu,waaminifu na wenye misimamo imara ya kusimamia mambo mema ya kuimarisha UWT na CCM hivyo mtu yeyote atakayewashawishi kutengeneza makundi ya kufanya kampeni za kusaka ungozi kwa sasa wamkatae na kutoa taarifa sehemu husika.

Kupitia ziara hiyo Tunu, aliwambia akina Mama hao ambao ni Wajumbe wa Kamati Tekelezaji ya UWT Wilaya hiyo kuendelea kuwa wabunifu wa miradi mbali mbali ya kujiingizia kipato ili kwenda sambamba na Sera ya CCM ya Siasa na Uchumi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items