Msemaji wa Yanga SC, Dismas Ten amesema kuwa wachezaji wanatumia muda mwingi kusafiri na kupata muda mchache wa kupumzika.
"Masaa 72 ambayo timu inabidi ipumzike, yanamalizika timu inaingia Uwanjani na mazingira yetu ya usafiri jinsi yalivyo si rafiki kwani wachezaji wanatumia muda wa kumpumzika wakiwa safarin," amesema.
Hadi sasa Yanga SC inaongoza Ligi Kuu Soka Tanzania (TPL) ikiwa na pointi 53 kibindoni na wakiwa wamecheza michezo 20, huku wapinzani wao wa jadi, Simba SC wakishika nafasi ya nne na pointi 33 lakini wakiwa wamecheza michezo 14 pekee.
