Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Potrabas Katambi ameweka wazi pamoja na kuwa na kazi nyingi alizonazo haweza kuibiwa Mke? Ametoa sababu tatu ambazo zitamfanya asiweze kuibiwa Mke.
Potrabas amesema kuwa ili usiibiwe ni lazima kwanza ufanye mazoezi, ili hata mwili wako ukiwa busy uwe na nguvu za kufanya mambo mengine vizuri.
"Cha kwanza fanya mazoezi, ili hata mwili wako ukiwa busy uwe na nguvu za kufanya mambo mengine vizuri, kwenye mazingira hayo utahisi unaibiwa kama kuna vitu vimepelea vitu vitatu vya upendo cha kwanza unapokuwa na Mpenzi wako, " alisema Katambi katika Mohojiano na A FM Redio ya Dodoma.
"Aonyeshe kweli una mjali na kwamba haumdanganyi basi kama kazi fulani fulani hivi zinazojenga upendo zifanyike vizuri na ukifanya vizuri ni udhibitisho kwamba yeye yuko peke yako maana yake ukishaiba iba kuna vitu fulani vinapungua na ukishapungua na wewe ule upendo wako utaonekana umepungua kwahiyo ataanza kuhisi mbona sio kama tulivyokuwa kipindi cha Girl Friend na BiyFriend? unajua hivi vitu havinaga siri sana."