Hakuna ushahidi wa ushirikiano wa Trump na Urusi


Ripoti iliyowasilishwa na mwanasheria maalum wa Marekani Robert Mueller haioneshi iwapo kuna ushahidi kwamba waendesha kampeni wa Rais Trump walishirikiana na Urusi katika kampeni ya uchaguzi wa Rais mnamo mwaka 2016.

Kwa mujibu wa muhtasari wa ripoti ya Robert Mueler uliondaliwa na mwanasheria mkuu wa nchini Marekani William Barr, kwenye barua yenye kurasa nne iliyowasilishwa kwa kamati ya wabunge wa Baraza la wawakilishi katika bunge la Marekani, Barr, ameeleza kuwa uchunguzi uliofanywa na Robert Müller haukuthibitisha iwapo Trump alifanya kosa la jinai.

Mwanasheria mkuu huyo amesema Mueller hakuwa na uhakika kwamba waendesha kampeni ya Trump walipanga au kuhusika na mpango wa serikali ya Urusi wa kuingilia kati ya uchaguzi wa Rais wa Marekani wa mwaka 2016. Akizungumzia juu ya ripoti hiyo Rais Trump amesema hana hatia.  Hatua hiyo inampa ushindi mkubwa wa kisiasa Rais Trump.

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema hitimisho la uchunguzi wa mwanasheria maalum Robert Mueller ni uthibitisho wa jumla kuwa Rais Donald Trump na waendesha kampeni yake wamevuliwa tuhuma mbaya mno na ni muhimu matokeo hayo kupokewa kwa furaha na Wamarekani wanaopenda ukweli na uadilifu uliokuwepo wakati wa uchaguzi. Pence ameiita siku iliyotolewa ripoti hiyo kuwa ni siku muhimu kwa taifa la Marekani, kwa rais Trump na Utawala wake.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items