Jinsi ya kuifanya jamii yako ikukubali kwa kile ukifanyacho

1. Jifunze kukumbuka majina ya watu. sio kila mtu anapenda aitwe “wee kaka/dada”, “ankoo”, “mzee”. Kukumbuka majina ya watu situ itakupa heshima, Bali pia utaonekana ni mtu makini na unayejali.

2. Kumsifia mtu anapofanya kitu kizuri (compliments). Nani hapendi kusifiwa?

3. Jifunze namna ya kufikisha habari mbaya/ ya kusikitisha kama msiba, ajali

4. Usipende kuangalia saa unapoongea na mtu hasa anapokuelezea tatizo lake. Badala yake kama unaona anakuchelewesha, tengeneza mazingira ya kupigiwa simu ili uondoke.

5. Jifunze kumjali kila mtu ambaye unafahamu na usiyemfahamu pia.

6. Jifunze kuepuka ugomvi. Na ukiingia kwenye ugomvi kwa bahati mbaya basi jifunze kushuka la sivyo hakikisha unashinda Ugomvi huo.

7. Jifunze kuwa msikilizaji mzuri. kumbuka, kila mtu anapenda kusikilizwa.

8. Jifunze kusema samahani na ahsante. Epuka kutumia maneno kama “najua” au “mimi pia” badala yake elezea unajua kiasi gani badala ya kutumia maneno hayo moja kwa moja!

9. Jifunze kuonyesha unakumbuka matatizo ya watu waliyokueleza hapo kabla na usisahau kuwauliza wamefikia wapi mnapokutana. Mfano kama alisema ana mgonjwa basi kumbuka kumuuliza hali ya mgonjwa. kumbuka Binadamu tunapenda kuonewa huruma.

10. Jifunze namna ya kumuonyesha ukarimu mgeni. Pia jifunze kuwa mgeni bora pale unapokaribishwa na mwenyeji wako

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items