Rais Magufuli ataka mashabiki wa Simba na Yanga waungane


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka mashabiki wa timu za Simba na Yanga waungane na kushangilia timu hizo zinapocheza kimataifa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Ikulu Dar wakati wa kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars na Bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi walioupata wikiendi iliyopita.

“Niwaombe Watanzania hasa mashabiki wa Yanga na Simba, inapocheza Simba katika michezo ya kimataifa basi tuishangilie Simba,pia inapocheza Yanga nayo tuishangilie, inawezekana hivi ndio vinatuchelewesha,” amesema Rais Magufuli.

“Nampongeza sana bondia Hassani ambaye nimefuatilia historia yake ameanza kufanya mazoezi kwenye matairi mpaka mikono ikawa na sugu hadi akampiga yule bondia akaanguka chini,”amesema Rais Magufuli .


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia