COSTECH yawanoa Waandishi wa habari


Na. Thabit  hamidu ,Zanzibar

Waandishi wa Habari Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya siku mbili na Tume ya Taifa ya Sayansi na Techologia (COSTECH) kwa lengo la kufikisha matokeo ya Tafiti  za Sayansi na Teknologia zinazofanywa Nchini.

Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Tume hiyo iliyopo Maruhubi Mjini Magharib Unguja na kuwajumuisha waandishi wa vyombo mbali mbali.

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara ya menejimenti ya Maarifa kutoka Tume hiyo Dk Joyce Nyoni aliwataka waandishi wa habari kushirikiana na watafiti mbalimbali ili kuipatia jamii taarifa juu ya tafiti na umuhimu wa utafiti unaofanywa Nchini.

Alisema wanachi wataelewa umuhimu wa tafiti za wataaalam endapo vyombo vya habari nzitasaidia kuwapa uwelewa juu ya umuhimu wa tafiti na kujua mambo mbali mbali ambayo yatawasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Aidha alibainiusha kuwa hakuna Nchi inayowqeza kuendelea bila utafiti hivyo ni vyema kwa watafiti kuwa karibu na kuongeza mashirikiano na wanahabari ili tafiti zinazofanywa kuwafikia wananchi.

“Tumeabaini kuna gape kubwa baina ya waandishi na watafiti hivyo tumeamua kuandaa mafunzo haya kwa lengo la kuwakutanisha na kutoa elimu kivipi wanaweza kufanya kazi kwa pamoja”alisema Dk Joyce.

Kwa upande wa waandishi wa habari walisema kuwa utofauti unapokuja pale wanahabari wanaposhindwa kushirikishwa na watafiti wakati tafiti zinapo kamilika.

“Tumeona tafiti nyingi zinafanywa ila watafiti huwa wagumu kueleza kile walichokibaini kwa wanahabari ili jamii ipate kujua” alisema Mwandishi wa Gazeti la Daily News Zanzibar Issa Yusuf.

Mafunzo hayo yaliwashirikisha watafiti mbali mbali wa mambo ya sayansi na teknologia na ubunifu.

 Kwa upande wao watafiti walisema kuwa huwa waoga kutoa taarifa mapema kwa waandishi wa habari ili tafiti za zisije kuharibiwa na kukosekana kwa majibu kabla ya kumaliza tafiti hizo.

Aidha walisema mara baada ya kupata mafunzo hayo kuwa wameona kuna umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili watafiti na wanahabari kushirikiana kwa pamoja katika kazi zao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia