Zitto afunguka suala la ACT Wazalendo kufutiwa usajili


Baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutoa muda wa wiki mbili kwa chama cha ACT Wazalendo , Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ameibuka na kutoa kauli.

Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe amesema kuwa hoja zote za msajili hazina mashiko na wataandika utetezi rasmi kama walivyotakiwa.

Zitto amesema sheria inawataka kuhakikisha wanachama wao hawavunji sheria na si watu baki, "Kama ilivyoandikwa kwenye barua ya Msajili, wale ambao wamefanya vitendo hivyo si wanachama wetu. Hatuna wajibu nao."
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items