Zitto ataja kitu ambacho ACT imevunja rekodi ya vyama vyote


Kiongozi wa cha cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa Chama chao  ndio chama cha kwanza kupata Hati Safi nchini .

Zitto akizungumza na Waandishi wa habari amesema kuwa wameshawaelekeza wa IT wa chama hicho kuwa Hati hizo waweke kwenye kwenye tovuti ya chama hicho ili wananchi waone.

"Na kwa taarifa tu Waandishi wa habari na Watanzani kwa ujumla tangu CAG aanze kukagua vyama, Chama chetu ndio chama cha kwanza kupata Hati Safi , ndio chama cha kwanza cha siasa katika nchi yetu kupata hati safi," alisema Zitto.

"Hati hizi tumewapatia na tumeshaelekeza idara ya IT taarifa zote hizi ziwekwe kwenye tovuti ya Chama wananchi waone ili kukata mzizi wa fitina ambazo Msajili wa Vyama atatuletea."
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items