Beyonce kuungana na kampuni ya Adidas


Malkia wa muziki Marekani Beyonce ametangazwa kuwa mshiriki wa kibiashara mpya wa kampuni ya Adidas, Queen Bey atakuwa mshiriki wa ubunifu katika kuachia line yake ya viatu, nguo na bidhaa nyingine za brand yake ya nguo ya Ivy Park.
.
"Huu ni ushirikiano wa kibiashara ni mkubwa sana katika maisha yangu," Beyoncé amefunguka kwenye Press Release aliyoiachia "Adidas imekuwa na mafanikio makubwa katika kusukuma mipaka ya ubunifu.

 Wote tuna falsafa inayohimiza ubunifu, ukuaji na uwajibikaji wa kijamii mbele ya biashara.Natarajia kuachia tena na kupanua brand ya Ivy Park kwa kiwango cha kimataifa chenye uhakikisho, wenye nguvu kiongozi."
.
Mwanzoni Beyonce alikua akifanya kazi na kampuni ya Topshop kuachia bidhaa zake za Ivy Park lakini baadae aliwapiga chini baada ya kuibuka tuhuma chafu za unyanyasaji wa kingono na ubaguzi dhidi ya Mmiliki wa kampuni hiyo.