Bunge lapitisha azimio la kutofanya kazi na CAG


Bunge limepitisha azimio la Kamati ya Haki, Maadili & Madaraka la kutoshirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad baada ya kukiri kuwa Bunge ni dhaifu na kusema hajutii na ataendelea kutumia neno hilo kwani kiuhasibu linamaanisha upungufu.

Mapema leo Kamati ya Maadili Haki na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwa kulidharau bunge.

 Kufuatia hatua hiyo Kamati imetoa mapendekezo ya Bunge kutofanya kazi na CAG,Prof.Asaad

Kamati hiyo imesema Prof. Assad alikiri mbele ya kamati kuliita Bunge dhaifu lakini alipingana na tafsiri ya neno 'dhaifu' iliyopo kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu inayosema 'goigoi, hafifu, isiyo imara' akisitiza kiuhasibu udhaifu ni 'upungufu'.

Utakumbuka CAG alipokuwa akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na alisema,'Kama tunatoa ripoti zinaonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, kwangu ni udhaifu wa Bunge,'.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items