Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuripoti kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia kauli yake kuwa "Bunge ni dhaifu". Lema ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, 2019 kwenye mkutano wa Bunge unaoendelea.
Mapema leo Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge pia imemtia hatiani Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa kulidharau Bunge kwa kuunga mkono kauli ya CAG kuwa Bunge ni dhaifu na hivyo apewe adhabu ya kutoudhuria mikutano miwili ya Bunge.
Vilevile Bunge la Tanzania limejadili na kupitisha hoja ya Kamati ya Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa halipo tayari kufanya kazi na CAG, Prof. Mussa Assad, kutokana na kauli yake aliyosema "Bunge ni dhaifu" na kwamba aligoma kuomba msamaha.
