Hivi ndivyo Rais Magufuli alivyomuita Lema


Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameitikia wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye msiba wa marehemu Tryphosa Simon Sanga (Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa) aliyefariki juzi jijini Dar Es Salaam.

Wakati Rais Magufuli akitoa pole kwa waliofika kwa ujumla, akamuita Lema na kumuambia "Lema njoo basi telemka hapa tusalimie."

Nae Mbunge huyo alishuka kwa haraka kwa kuuheshimu wito huo kwa kushuka eneo alilokuwepo lilikuwa na kilima huku akisema yeye ni komandoo yaani eneo hilo hawezi kuanguka.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items