Ommy Dimpoz afunguka kuhusu kufanya show kwa sasa



Msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz amefunguka kuwa kwa sasa bado hajarudi rasmi kwenye kufanya show za majukwaani.

Muimbaji huyo akiongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, amesema sababu ni kutokana na kutakiwa kurudi tena hospital kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi ili kama ataruhusiwa ataweza kufanya hivyo.

"Bado sijarudi rasmi kufanya show kwenye majukwaa mbalimbali kwani natakiwa nirudi tena hospital kwa ajili ya vipimo na daktari ndiyo atasema kuwa kwa sasa naruhusiwa au vipi" amesema Ommy.

Kwa sasa msanii huyo ameachia video ya wimbo wake mpya "You Are The Best" wiki iliyopita ambayo mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube imeshatazamwa zaidi ya mara 720.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items