Wiki hii Ethiopia kutoa ripoti ya Boeing 737 MAX iliyopata ajali


Ethiopia imesema kuwa haitatoa ripoti ya awali kuhusu sababu za ajali ya ndege aina ya Boeing 737 MAX ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines, ambayo iliua watu 157 Machi 10, lakini inaweza kutoa ripoti hiyo baadaye wiki hii.

Ndege hiyo yenye chapa 302 iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa kwenda Nairobi ilianguka kwenye shamba, karibu na mji mkuu wa Ethiopia, dakika sita tu baada ya kuruka. Abiria kutoka mataifa zaidi ya 30 walikuwa kwenye ndege hiyo waliangamia.

Ajali hiyo ilitokea miezi mitano baada ya ajali nyingine pia iliyohusisha Boeing 737 MAX 8. Ndege hiyo ya shirika la ndege la Indonesia la Lion Air ilianguka mnamo mwezi Oktoba mwaka jana na kuua watu 189. Ajali ya Boeing 737 MAX ya Shirika la ndege la Ethiopian Airlines ilisababisha ndege za aina hiyo kupigwa marufuku kusafiri katika nchi mbalimbali duniani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items