Iran imesema itaongeza urutubishaji wa madini ya uranium baada ya siku 60, mwaka mmoja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo wa kimataifa.
Rais Hassan Rouhani amesema baada ya siku 60 Tehran itaongeza zaidi urutubishaji wa madini ya uranium yanayotengeneza nyuklia ambayo yamezuiwa na mkataba huo.
Mkataba huo unalenga kukabiliana na utengenezaji wa nyuklia ili iweze kuondolewa vikwazo vya misaada , lakini uhasama umeongezeka tangu Marekani ijiondoe.
Uchumi wa Iran umeyumbishwa na vikwazo vipya vya Marekani dhidi yake.
