TRA yapewa vifaa vya kisasa kwaajili ya kusajili walipa kodi na Denmark


Serikali ya Denmark kwa kushirikiana na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji,  wametoa mashine za kutengenezea vyeti vya walipa kodi, kwa vituo kumi na tatu(13) vilivyojengwa ndani ya halmashauri za mikoa ya Dodoma na Kigoma.

Vitakavyo tumika na Mamlaka ya  Mapato Tanzania, TRA, kutoa elimu kwa mlipa kodi, na vyenye thamani ya zaidi ya milioni mia moja sitini na saba(167), lengo  likiwa ni kuboresha mazingira ya biashara na udhibiti wa upotevu wa mapato.

Akipokea vifaa hivyo Jijini Dodoma, katibu mkuu,  Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Joseph Nyamhanga, amesema msaada huo utasaidia katika juhudi za serikali katika mapambano na kudhibiti upotevu wa mapato.

Amesema  vifaa hivyo itakuwa msaada mkubwa katika kuandaa takwimu zitakazopatikana ndani ya vituo vya uwekezaji vilivyojengwa katika halmashauri za mikoa ya Dodoma na Kigoma, ambazoo pia zinazohusiana na biashara na uwekezaji, ikiwa ni pamoja na kujua bidhaa zinazozalishwa katika maeneo husika.

“Tumejenga vituo vya kutoa elimu kwa mlipa kodi, kwa msaada huu utasaidia tujue takwimu sahihi zitakazopatikana ndani ya vituo hivi tulivyovijenga ili kutoa elimu kwa mlipa kodi ambapo kwa kuanza tumejenga halmashauri za mikoa ya Dodoma na Kigoma na baadaye tunaenda katika mikoa mingine” amesema Nyamhanga.

Amesema vituo hivyo ambavyo vitatumika kutoa elimu kwa mlipa kodi, vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi waliokuwa wakitoka halmashauri moja kwenda makao makuu ya mikoa kupata huduma hiyo.



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia