Kocha wa Yanga SC arejea kwao


Kocha mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera leo amekwea pipa kurejea kwao DR Congo huku akimuachia majukumu ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City msaidizi wake Noel Mwandila.

Jana Zahera aliongoza kikosi chake kucheza mchezo wake wa 36 mbele ya Ruvu Shooting na waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Pappy Tshishimbi.

Zahera amesema kuwa anatarajia kurudi kabla ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City hivyo majukumu yote ya maandalizi  kamuachia msaidizi wake ashughulike nayo.