Serikali yakanusha biashara milioni 1 kufungwa nchini


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amekanusha leo Bungeni kuwa sio kweli kwamba kuna biashara milioni 1 zimefungwa mwaka huu.

Badala yake, amesema kati kipindi cha kuanzia mwezi wa 7-2018 hadi mwezi wa 4-2019 jumla ya biashara zilizofungwa nchini ni 17,252 huku biashara mpya zilizofunguliwa zikiwa ni 147,818.

Naibu Waziri Kijaji amehoji kuwa kama biashara zinazofungwa nchini zingekuwa nyingi kuliko zinazofunguliwa basi Mamlaka ya Mapato (TRA) ingewezaje kukusanya mapato inayokusanya leo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia