Waziri wa nishati atumbuliwa kisa mgao wa umeme


Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemfukuza kazi waziri wa nishati, Joram Gumbo kwa sababu ya tatizo la kukatika umeme mara kwa mara tangu mwaka 2016.

Nafasi ya waziri huyo amepewa naibu waziri wa usafirishaji na miundo mbinu Forune Chasi.

Gumbo sasa amepewa wadhifa wa kuwa waziri katika ofisi ya rais ,kufuatilia utendaji na utekelezaji wa idara za serikali.

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali amesema siku ya jumatatu kuwa umeme ambao umekuwa ukikatika kwa saa tano au nane kutokana na upungufu wa maji katika mtambo mkubwa wa uzalishaji umeme.

Siku ya jumatatu , kampuni ya uzalishaji umeme inayomilikiwa na serikali ilitangaza kuwa umeme utakatika kwa saa tano mpaka nane. Vilevile machimbo ya migodi yatahathirika na kukatika huko kwa umeme.

Mamlaka inalaumu kuzimika au kukatika kwa umeme huo kutokana na mtambo wa uzalishaji umeme kuzalisha umeme kwa kiwango kidogo kutokana na ukame ambao umesababisha maji kupatikana kwa kiwango kidogo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia