Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mamlaka ya mapato TRA mkoani Arusha imetoa onyo kwa baadhi ya vishoka wanaowatapeli wafanyabiashara kupitia mgongo wa TRA waache kufanya hivyo mara moja kwani watachukulia hatua kali za kisheria kwani wanakwamisha ulipaji kodi kwa hiari.
Kaimu Meneja wa TRA Irine Donald amesema hayo jana katika soko la Tengeru ambapo alizungumza na walipa kodi katika wiki ya mlipa kodi ,ambapo amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaofahamika kama vishoka ambao hufika TRA na kufanya udanganyifu kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujipatia faida huku wakiwaumiza wafanyabiashara.
Mkuu wa Wilaya ya Meru Jerry Muro amesema kuwa wafanyabiashara wanapaswa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangaia maendeleo ya nchi na kuiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.
Kwa upande wao wafanyabiashara waliofika kupata elimu ya mlipa kodi Magreth Pallangyo amelalamikia uchafu wa soko la tengeru licha ya kulipa ushuru kwa Halmashauri hiyo hivyo wameiomba serikali itatue changamoto hiyo ili waweze kulipa kodi stahiki.
