Mgombea wa upinzani ambaye ameondolewa katika nafasi yake ya umeya baada ya kutolewa uamuzi tata wa kurejewa kwa uchaguzi wa jiji la Istanbul, Uturuki anafanya mazungumzo na kiongozi wa Chama yenye lengo la kujadili mkakati.
Chama kikuu cha upinzani cha CHP kimelaani uamuzi huo uliotolewa na bodi ya juu kabisa ya uchaguzi wa kurejea uchaguzi kwa kusema "Sio kwa kidemokrasia na wala hauna uhalali". Ekrem Imamoglu, ambaye alishinda katika uchaguzi uliovurugika, amekutana na kiongozi wa chama chake cha CHP, Chifu Kemal Kilicdoroglu na baadaye atakutana na kiongozi mwingine wa Good Party Meral Aksener.
Mazungumzo hayo yanafanyika siku moja baada ya baraza la juu kabisa la uchaguzi YSK kutaka kurejewa tena kwa uchaguzi wa Jiji la Istanbul, baada ya Chama tawala cha Rais Recep Tayyip Erdogan kulalamika kuhusu kile walichokiita ukiukwaji na kuwepo kwa vitendo vya uhalifu wa kupangwa.
