Waandishi wa Reuters waachiwa huru



Waandishi wawili wa Shirika la habari la Reuters, Wa Lone, 32 na Kyaw Soe Oo 28, wameachiwa huru na mamlaka ya Myanmar baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba Disemba mwaka jana.

Waandishi hao wameachiwa sambamba na wafungwa wengine 6,518 kwa msamaha wa rais.
Waandishi hao walikamatwa kwa kukutwa na nyaraka za serikali kinyume cha sheria.

Walipatikana na hatia Septemba mwaka jana na kuhukumiwa kwenda jela miaka saba katika kesi ambayo ilizusha maswali mengi juu ya hatua za Myanmar kuelekea katika demokrasia na kuzusha malalamiko kutoka kwa wanadiplomasia na watetezi wa haki za binadamu.

o.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia