Na Clavery Christian Bukoba.
Taasisi ya RSA inayojishughulisha na masuala ya kutoa Elimu kwa jamii juu ya usalama barabarani imesema imeandaa mpango ambao utaweza kusaidia kupunguza ajali za barabari hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Bi. Iren Mselemu Barozi wa usalama barabarani kutoka RSA Tanzania wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani yaliyofanyika mkoani Kagera kitaifa.
Akisoma ujumbe wake mgeni rasmi katika kufungua mafunzo hayo, Robert Rubimbi ambaye ni mkaguzi wa ndani wa serikali amesema kuwa ni vema wahusika wa barabara kuhakikisha wanaweka alama na vibao vya kuonyesha alama na ishara mbalimbali barabarani ili kuweza kuzuia hajali zinazoweza kuepukika.
Aidha washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Polisi wa usalama barabarani, Waandishi wa Habari, tan road, tarula na jeshi la zimamoto wamesema kuwa mafunzo hayo yataweza kuwasaidia watumiaji wa vyombo vya moto na jamii kwa ujumla kuelewa na kuzingatia sheria na kanuni pamoja na matumizi bora ya barabara.

