WHO yathibitisha Algeria na Argentina kutomeza malaria


Shirika la Afya Duniani WHO limethibitisha kuwa Algeria na Argentina zimetokomeza malaria baada ya nchi hizo kutoshuhudia maambukizi ya ugonjwa huo katika miaka mitatu iliyopita.

Algeria ni nchi ya pili ya Afrika kutambuliwa na WHO kutokuwa na ugonjwa wa Malaria baada ya Mauritius, iliyothibitishwa mwaka 1973.

Kwa upande wa Argentina imekuwa ni nchi ya pili katika bara la Amerika kuthibitishwa kutokomeza ugonjwa huo katika miaka 45 iliyopita baada ya Paraguay mwezi Juni mwaka jana.