Argentina na Uruguay zapata tena umeme baada ya kiza cha muda mrefu

Wasambazaji wa umeme nchini Argentina na Uruguay jana usiku wamesema kwamba umeme umerudishwa takriban kote katika nchi hizo mbili ikiwa ni karibu siku nzima ya kushuhudiwa kupotea kwa umeme uliowaacha mamilioni ya wakaazi kukosa huduma hiyo Amerika ya Kusini.

Kiasi watu milioni 47 katika nchi hizo mbili wengi sasa wamepata umeme kwa mujibu wa makampuni makubwa ya usambazaji umeme Argentina Edesur na Edenor pamoja na wenzao wa Uruguay UTE.

Nchi hizo mbili zimekaa bila ya umeme kwa kipindi cha saa 15 jana Jumapili.Waziri wa nishati wa Argentina Gustavo Lopetegui katika mkutano na waandishi habari amesema mfumo wa nguvu za umeme ulizimimwa kutokana na kugunfdulika hitilafu.

Ingawa pia waziri huyo hakuondowa uwezekano wa tukio hilo kusababishwa na shambulizi la mtandao,uchunguzi bado unaendelea.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia