Viongozi waitisha maandamano ya usiku nchi nzima Sudan

KhartoumViongozi wa maandamano nchini Sudan wametowa mwito wa kuanza kufanyika maandamano na matembezi ya usiku katika mji mkuu Khartoum na maeneo mengine ya nchi hiyo kufuatia mvutano mkali uliopi na baraza la kijeshi linaloshikilia madaraka.

Viongozi wa maandamano wamesema leo kwamba wameanza kuyatanua mapinduzi ili kuwashinikiza majenerali wa kijeshi kuyakabidhi madaraka kwa uma pamoja na kulaani hatua ya jeshi ya kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji katika mji wa Khartoum mwanzoni mwa mwezi huu.

Watu wasiopungua 128 wamefariki tangu lilipotokea tukio hilo Juni 3 la kuwatawanya waandamanaji. Kundi linalowawakilisha waandamanaji ,linalojulikana kama vikosi vya azimio la uhuru na mabadiliko, linasema maandanao ya usiku yataanza Jumanne kesho na matembezi yatafanyika alhamisi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia