DC Ilala amuagiza RPC kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kubaini waliomua Mwanafunzi wa Chuo Kikuu


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza RPC wa Ilala Kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kuwatafuta wahalifu waliomvamia kumchoma visu na kisha kumsababishia mauti binti Anifa Mgaya mwanafunzi wa stashahada ya maabara kutoka chuo kikuu cha Kampala kilichopo Gongo la Mboto

Kabla ya umauti kumfika Anifa (pichani juu) alichomwa visu viwili na watu wasiojulikana majira ya saa mbili usiku jirani na geti la kuingia Chuo kikuu cha Kampala.

Marehemu alianguka chini na kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ambao baadhi walikuwepo eneo la tukio. Baadae wakajitokeza baadhi ya wanafunzi kumpatia msaada wa haraka kumfikisha hospitali ambapo hata hivyo tayari mauti yalishamfika binti huyo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia