IGP sirro awaonya vikali Askari


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewataka Maofisa na askari kuhakikisha wanaendelea kutimiza wajibu wao kikamilifu na kutokujiingiza kwenye masuala ya uhalifu ikiwemo kushiriki kwenye wizi wa dhahabu sambamba na uhujum uchumi.

IGP Sirro, ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa akizungumza na Maofisa na Wakaguzi wa Jeshi hilo ambapo amesema kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa askari anayeshiriki kwenye uhalifu ikiwemo kufukuzwa kazi pamojana kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha suala la uchaguzi linafanyika kwa amani na utulivu na kwamba amewahakikishia wananchi usalama wao na mali zao na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa sahihi za
uhalifu na wahalifu.

Kwa upande wake kamishna wa kamisheni ya ushirikishwaji wa jamii CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa, uhusiano kati ya jeshi la polisi na jamii umeendelea kuimarika nchini kutokanana taarifa zinazoendelea kutolewa kutoka kwa raia wema na wapenda amani.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items