Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema wabunge 48 watakwenda kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika Fainali za Mataifa ya Afika (AFCON) zinazofanyika nchini Misri wakiambatana na Peter Mollel maarufu Pierre Konki Liquid.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Ndugai amesema wataambatana na mchekeshaji huyo katika fainali hizo huku akiwataka wabunge zaidi kujiandikisha ili kwenda Misri.
Utakumbuka hapo awali Waziri Mkuu wa Kasimu Majaliwa tayari alisema kuwa Pierre Konki Liquid ataambatana na washabiki wa Taifa Stars kuelekea nchini Misri kwenye fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19, 2019.
