Beki wa Azam FC, David Mwantika ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazoanza kutimua vumbi Juni 21 mwaka huu nchini Misri.
Mwantika ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wameitwa kwenye kikosi cha awali kabla ya kutemwa katika mchujo wa kupata wachezaji 23, anakwenda kuziba pengo la Agrey Moris ambaye amepata majeraha wakati wa mechi za maandalizi.

