Umoja wa Mataifa umesema leo kuwa nchi zinazoendelea zinabeba mzigo wa mzozo wa wakimbiuzi duniani na zinawapa hifadhi wengi wa watu milioni 70.8 wanaokimbia vita na mateso nchini mwao.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia Wakimbizi - UNHCR limesema katika ripoti yake ya kila mwaka kuwa nusu ya watu waliolazimishwa kuyahama makazi yao duniani ni watoto, na kwamba idadi ya waliokimbia makwao katika mwaka wa 2018 ndiyo kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa kwa karibu miaka 70.
Kamishna wa UNHCR Filipo Grandi amesema kwa bahati mbaya hali inachukua mwelekeo usio sahihi, na kwamba imeibuka mizozo mpya ambayo inaongeza idadi ya wakimbizi juu ya waliokuwepo ambao tayari ni wengi.
Grandi amepinga dhana kwamba wote wanaozihama nchi zao ni wakimbizi wa kiuchumi. Kiongozi huyo wa UNHCR amesema matatizo ya wakimbizi yanaongezeka kwa idadi yao na kwa muda wanaoishi uhamishoni. Amesema asilimia 80 wamekuwa wakimbizi kwa zaidi ya miaka 5.