Mbunge mweusi wa Afrika Kusini amejitetea kuwa alimpiga ngumi mbunge mwanamume baada ya kudaiwa kumtusi matusi ya ubaguzi wa rangi.
Phumzile van Damme kutoka chama cha upinzani cha Democratic Alliance amesema kuwa alijipata katika mzozo na mwanamke mzungu katika mji wa V&A Waterfronyt uliopo Cape wakati mwanamme mzungu alipotishia kuleta ghasia na kutumia lugha chafu alipokuwa akimzungumzia akimtaja kama "wewe mweusi".
Mji wa V&A Waterfront, ambao ni kitovu kikuu cha utalii, umeomba radhi kwa tukio hilo.
Bi van Damme hakufurahia namna alivyotendewa na afisa wa usalama aliporipoti kwake tukio.
" Tunasikitishwa na tukio hili, ambalo hatukulishighulikia kwa malengo muhimu ,kwa heshima na huruma ," ulieleza mji wa kitalii wa V&A Waterfront kwenye ukurasa wake waTwitter.
Bi van Damme amesema kuwa alikuwa amesimama kwenye mstari katika duka la bidhaa mbalimbali alipolazimika kuzozana mwanamke huyo ambaye anayedaiwa kuwambia kuwa " atamsukuma kando".
"Halafu nilipokwenda nje, alikuwa amesimama pale na familia yake katika hali ya kunitisha. Na ndipo nilipomsogelea na kumwambia, 'kwanini unaniangalia hivyo kwa kunitisha ?' Halafu akasema, 'ni kwasababu wewe ni mweusi', Alisema van Damme katika video aliyoiweka kwenye ukurasa wake Twitter.
Alisema kuwa manamme, ambaye alikuwa na nwanamke, "alikuwa natishi kuzua ghasia, kwa hiyo katika hali ya kujilinda nilimpigga ngumi kwenye kichwa chake".
Bi van Damme amesema kuwa anakubali kutoa msama kwa V&A Waterfront na jukumu lao la kutovumilia tabia na mienendo isiyokubalika inayofanywa na wafanyakazi wake.
Amesema, hata hivyo ametishia kupeleka mashtaka kwa polisi.
Visa vya ubaguzi wa rangi vimekuwa vikiendelea kugonga vichwa vya havbari nchini Afrika Kusini.
Matamshi na mashambulio ya mwili ni miongoni mwa matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa licha ya kipind cha ubaguzi wa rangi kuripotiwa kumalizika baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hayati Nelson Mandela kuchukua mamlaka 1994.
Moja ya matukio hayo ni kupigwa kwa mtangazaji wa Televisheni na redio nchini Afrika Kusini mweusi ambaye alisema kuwa alikuwa muathiriwa wa shambulio lililochochewa na ubaguzi wa rangi baada ya kusimamisha gari lake kwa ajili ya kulisaidia kundi la wazungu ambao gari lao lilikuwa limepinduka.
Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio Mwaka jana.
Yeye na marafiki zake wawili wa kike waliitwa "nyani", alisema. Walipoulizwa ni kwanini wanatukanwa, walipigwa hadi wakapoteza fahamu.
Taarifa juu ya shambulio hilo zilizua hasira miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.