Rais Trump aanzisha kampeni ya kuchaguliwa tena 2020

Rais Donald Trump amezindua kampeni ya kuwania muhula wa pili katika mkutano uliogubikwa na malalamiko na matamshi ya visasi kuliko kubainisha ajenda yake kwa muhula wa pili.

Jumanne usiku katika mji wa Orlando jimboni Florida, Trump alilalamika kwamba amekuwa chini ya mashambulizi tangu siku ya kwanza ya urais wake kutoka kwa kile alichokitaja kuwa "vyombo vya habari za uzushi" na uwindwaji haramu wa kisiasa, ambavyo vimejaribu kumtuliza yeye na wafuasi wake.

Trump alichora taswira ya kutia wasiwasi ya nini kinaweza kutokea ikiwa atashinda katika uchaguzi huo wa 2020, akiuambia umati wa wafuasi wake kwamba "Wademocrat wanataka kuwaharibu, na wanataka kuiharibu nchi yetu kama tunavyoijua."

Timu ya kampeni ya makamu wa zamani wa rais Joe Biden kupitia taarifa ilisema nchi inakabiliwa na chaguo la ama kumfanya Trump kuwa punguani au kumuacha aubadilishe kimsingi na milele mwenendo wa taifa hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia