Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema watu 691 wameuawa na wengine 4,012 walijeruhiwa katika vita karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Wanamgambo ambao wanapigana na majeshi ya serikali wakiongozwa na Khalifa Haftar,wameongeza kampeni zao za kijeshi tangu mapema Aprili ili kuchukua mji wa Tripoli, ambapo serikali inayoungwa mkono na umoja wa mataifa (UN) iko.

