Umoja wa Wanawake wa Tanzania CCM wilaya ya Dodoma Mjini wameanza ziara yao ya kutembelea Kata 41 za Wilaya hiyo yenye lengo la kutoa elimu ya kiuchumi na viwanda kwa wanawake.
Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Winfrida Kaliyo amesema elimu itakayotolewa ni pamoja na elimu ya viwanda vidogovidogo, Kilimo na fursa za mazingira.
Nae Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa amewataka wanawake na vijana kujitokeza kwa wingi katika kupata elimu ya mifuko ya uwezeshaji kama SIDO, Maendeleo ya Jamii.
"Ndugu zangu tumekuja na watalaamu wetu kutoka Jiji na SIDO watawapa elimu, Niwasihi baada ya hapa mtaunda vikundi vyenu ambavyo vitawapa fursa ya kuchukua mikopo inayotolewa Halmashauri ya jiji la Dodoma kwa ajili yenu Wanawake, Vijana na Walemavu," Amesema Diana Joseph Madukwa.
Kwa upande wao wananchi waliojitokeza kwenye semina hiyo wameushukuru Umoja wa Wanawake wa Tanazania (UWT) huo kwa kuandaa ziara hiyo yenye lengo la kuwakwamua kiuchumi.

