Na Thabit Hamidu,Zanzibar.
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Rizik Pembe Juma amewataka walimu wakuu katika skuli za Msingi na Sekondari Nchini kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza michezo maskulini.
Amesema Walimu wakuu wanapaswa kuwa mstari wa mbele ili kuhakikisha masomo ya michezo katika skuli yao yanapewa kipaumbele.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na walimu Wakuu wa Skuli za Msinngi na Sekondari Unguja mara baada ya kupokea msaada wa Vifaa mbalimbali vya michezo kutoka Kwa taasisi ya Zan Education and Sports (ZESI).
Hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika katika viwanja vya Wizara hiyo Mazizini Mkoa wa Mjini Unguja.
Waziri Pembe alisema Walimu wakuu wanatakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhamasisha michezo kuanzia maskulini.
“Ni lazima kwa pamoja baina yetu na nyinyi kwa pamoja kuunga mkono jitihada za Serikali kwa hali na Mali ili somo la michezo lifungishwe ipasavyo na masomo mengine” alisema Waziri Pembe.
Alieleza kuwa kwa Mwalimu yoyote atakae kwamisha au kutounga mkono kusomeshwa kwa somo la michezo maskulini atachukuliwa hatua.
“Tunafahamu kwamba kuna baadhi ya walimu katika baadhi ya skuli hawaungi mkono somo la elimu kwa michezo pia kuna kuwavunja moyo wanafunzi wanaofanya michezo tutahakikisha tunawashughulikia ipasavyo” Alieleza Waziri.
Katika maelezo yake waziri alimwagiza Katibu Mkuu wa WIzara na Afisa Utumisha kufuatilia kwa karibu walimu ambapo wanakwamisha kusomeshwa kwa somo la Michezo maskulini ili hatua zichukuliwa Dhidi yao.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Zesi Ameir Mohameed Makame akikabidhi vifaa hivyo vya michezo maskulini kwa Waziri alisema kuwa Misaada huo unalengo la kusaidia na kukuza michezo maskulini ili kuibua vioaji vya vijana pindi wakiwa ngazi za skuli.
“Tumeamua kuungana kwa pamoja na wadau wa maendeleo ili kusaidia kuinua vipaji vya vijana wetu wakiwa maskulini” alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Seti ya Jezi kwa skuli tano,Mipira ya basketball, Mipira ya Tennis pamoja na meza za kuchezea michezo wa Table Tennis.
Msaada huo wenye thamani ya Zaidi ya Dola Elfu 5 umetolewa na wadau wa maendeleo kutoka nchini Demark.
