Na Timthay Itembe-Mara
WALIMU wilayani Tarime mkoani Mara wametakiwa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwa lengo la kuwapata viongozi Bora na wala sio Bora viongozi.
Hayo yalibainishwa juzi na Mshauri wa shirika la Mujata, Taifa,Peter Kayemba kwenye halfa ya kuwashukuru walimu kwa kazi ngumu waliyonayo ya kuwafundisha na kuwapa taaluma ya Elimu wanafunzi hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nkende.
Kayemba alisema kuwa walimu ni moja ya washiriki wakubwa wa uchaguzi kwahali hiyo wanatakiwa kushiriki chaguzi kwa ubora zaidi ili kumpata kiongozi bora na sio Bora kiongozi.
Naye mgeni rasimi wa halfa hiyo Chomete Samweli kwa niaba ya mkuu wa wilaya Tarime,Charles Kabeho alisema kuwa walimu wanatakiwa kushirikiana na jamii katika kufanikisha taaluma kwa wanafunzi. Pia Samweli aliongeza kuwa kuna haja jamii kujenga tabia ya kuwekeza kwa watoto badala ya kuwafanya mitaji hususani watoto wa kike kwani elimu ni msingi wa maendeleo.
