Timu ya Ufuatiliaji yakerwa na kususua kwa ujenzi wa Zahanati ya Matale Simiyu


NaAngela Msimbira-SIMIYU

Timu ya ufuatiliaji inayoshughulika na Mradi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR- TAMISEMI imekerwa na kusuasua kwa ujenzi wa Zahanati ya Matale, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akiongea kwa niaba ya Timu hiyo Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda amesema ujenzi wa zahanati hiyo umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya
vitu vingi kutokamilika na jengo hilo kutotumika licha ya kutakiwa kuanza kutoa huduma za mama na mtoto katika jengo hilo.

Ameyataja maeneo ambayo hayajakamilika kuwa ni uwekaji wa milango, ufungaji wa gata za kuvunia maji, uwekaji wa madirisha ya alluminium, uwekaji wa mfumo wa umeme, uwekaji wa marumaru upande wa vyooni,uchimbaji na ujenzi wa mashimo ya maji taka, uwekaji wa masinki wakati fedha zote zilitolewa kwa ajili ya ujenzi ambapo ujenzi huo ulikuwa unatakiwa kukamilika juni, 2018.

“Ni jambo la kushangaza kuona Zahanati iliyotakiwa kuanza kutumika tangu 2018 mpaka leo haijaanza kufanya kazi japokuwa Serikali imeweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo, suala hili halipendezi na linarudisha nyuma maendeleo kwa jamii” amesisitiza Bi. Atinda.

Amesema kuwa timu imegundua kuwa kuna matumizi ya fedha yasiyofuata miongozo yaliyofanywa wakati wa ujenzi wa miundombinu ya Zahanati hiyo ambapo taarifa zinaonyesha kuwa Fundi wa ujenzi amelipwa zaidi ya Tsh. Milioni 5 kati ya 6 alizotakiwa kulipwa wakati sehemu kubwa ya ujenzi huo haujakamilika.

Bi. Atinda ameiagiza Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa jengo hilo na kuanzakutumika ifikapo tarehe 30 juni, 2019 na kutumia fedha zilizopelekwa na TAMISEMI katika robo ya nne ya mwaka 2018/2019 kufanya usimamizi wa
vituo vyote vya kutolea huduma za afya 38 vilivyofanyiwa maboresho chini


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia