Washukiwa watatu wa ugaidi watiwa hatiani Kenya

Washukiwa watatu wa ugaidi akiwemo raia wa Tanzania wamepatikana na hatia ya kufanya shambulio la kigaidi la mwaka 2015 lililotokea kwenye chuo kikuu cha Garissa na kuwaua zaidi ya watu 140.

Kesi hii ilianza kusikilkizwa tangu mwaka 2016. Hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Francis Andayi aliamuru kuwa watatu hao wamepatikana na hatia ya kufanikisha shambulio la kigaidi.

Mohamed Abikar, Hassan Hassan na Rashid Charles Mberesero ndio waliofikishwa mahakamani hii leo jijini Nairobi. Sahal Diriy aliyejulikana pia kama Sahali Diriye aliachiliwa. Hussein Osman Dagane aliyekuwa bawabu wa chuo hicho cha Garissa aliachiliwa kwa ukosefu wa ushahidi. Wote walifika mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na watu 22 walitoa ushuhuda wao.

Mashtaka yaliyowaandama ni pamoja na kuhusika na ugaidi, kupanga njama ya kigaidi na kuwa wanachama wa kundi la kigaidi. Mberesero ambaye ni raia wa Tanzania alishtakiwa pia kwa kuwa ndani ya mipaka ya Kenya kinyume na sheria.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia