Wawezeshaji kutoka TASAF Makambako wanolewa



Na Amiri kilagalila-Njombe

Katika kuhakikisha Mpango wa Kunusuru kaya Masikini TASAF Unafanikiwa kwa kiwango kikubwa mkoani Njombe Mafunzo maalumu kwa Wawezeshaji wa Mpango huo yamefanyika katika halmashauri ya Mji wa Makambako ili kuhakikisha wanufaika wa mpango huo wanajiunga katika Vikundi mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na Umaskini.

Neema Chaula ni Mratibu wa Tasaf halmashauri ya mji wa Makambako amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Wawezeshaji wa Mpango huo kuhusu suala la kuhamasisha Wanufaika wa Mpango huo kujiunga katika Vikundi mbalimbali ambapo wanaamini kwa kufanya hivyo kutawasaidia wanufaika kujikwamua kiuchumi kwa kuunganisha nguvu zao pamoja na kufanya matumizi sahihi ya fedha zitokanazo na Mpango huo wa Kunusuru kaya Masikini hapa nchini.

Pamoja na hayo Neema amesema changamoto kubwa kwa baadhi ya Wanufaika wa Mpango huo ni kutumia fedha vibaya kwa kuwa wengi wamekuwa wakitumia katika ulevi huku akitoa wito kwa walengwa kuwa makini  na Fedha hizo kwani Malengo ya Serikali ni kutaka kuziinua kaya Masikini

Masinde Masinde ni Muwezeshaji wa Tasaf kutoka Halmashauri ya Mji Makambako na baadhi ya Washiriki wengine wanasema kuwa kazi waliyonayo hivi sasa kama wawezeshaji ni kuhamasisha wananchi kujiunga katika Vikundi ili Waweze kujikwamua kiuchumi.

Mpango wa Kunusuru kaya Masikini Tasaf ulianzishwa kwa lengo la kuzisaidia kaya Masikini hapa nchini ili ziweze kuinuka na kujitegemea kiuchumi ambapo Mpango huu umekuwa ukitekelezwa nchi nzima.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia