Loading...

Jul 14, 2019

Licha ya kuibuka na ushindi KMC yatupwa nje Kagame Cup

Timu ya KMC imeweza kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame lakini imetupwa nje ya michuano hiyo.

Bao pekee la kiungo mshambuliaji Hassan Salum Kabunda dakika ya 30 limeipa ushindi wa 1-0 KMC dhidi ya wenyeji, Rayon Sports Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Mechi nyingine za Kundi A TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeichapa 6-1 Atlabara ya Sudan Kusini na Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Kwa matokeo hayo, TP Mazembe na Rayon Sport zimemaliza na pointi sawa, sita kila moja na kufuzu Robo Fainali kwa pamoja, huku KMC na Atlabara zikifanya safari kurejea ‘makwao’.

TP Mazembe na Rayon Sport zinaungana na wenyeji wengine APR, mabingwa watetezi, Azam FC ua Tanzania pia, KCCA ya Uganda na Green Eagles ya Zambia zilizotangulia Robo Fainali kutoka Kundi B na C.

Michuano hiyo itahitimishwa leo kwa mechi za Kundi D kati ya mabingwa wa zamani, Gor Mahia ya Kenya dhidi ya KMKM ya Zanzibar kuanzia Saa 8:00 mchana kabla ya Port ya Djibouti kukipiga na Manyema Union ya DRC kuanzia Saa 10: 30 jioni.

Kwa sasa Gor Mahia inaongoza Kundi D ikiwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Manyema Union ya DRC yenye pointi tatu sawa na Port, wakati KMKM inashika mkia ikiwa haina pointi.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger