Wanadiplomasia wa Uturuki wameshambuliwa mkoani Erbil nchini Iran na watu waliokuwa na silaha.
Shambulizi hilo limelaaniwa na mataifa tofauti ikiwemo pia Uingereza na Marekani.
Shambulizi hilo liliwalenga wanadiplomasia wa Uturuki katika mgahawa mmoja Jumatano na kupelekea mmoja miongoni mwa wanadiplomasia hayo kufariki.
Mwili wake umewasili Uturuki kwa ajili ya mazishi.
Baada ya shambulizi, mwili wa mwanadiplomasia aliefariki ulipelekwa katika hospitali ya Rizgari kwa ajili ya uchunguzi.
Muakilishi wa Uingereza Umoja wa Ulaya na Marekani Alan Duncan amelaani tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Uingereza imetoa mkono wa pole kwa Uturuki kufuatia maafa ya mwanadiplomasia wake nchini Irak.
Mike Pompeo pia amekemea shambulizi hilo.