Rais Putin na Macron wajadili muafaka wa nyuklia wa Iran

Rais wa Urusi Vladmir Putin na kiongozi wa Ufaransa Emmanuel Macron wamekubaliana leo kuhusu haja ya kuweka pamoja juhudi zao ili kuuokoa mkataba wa nyuklia wa Iran kufuatia miezi mingi ya mivutano.

Taarifa kutoka Ikulu ya Urusi imesema Putin na Macron wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kukubaliana kuwa muafaka huo wa Iran ni sababu muhimu ya kuhakikisha usalama katika Mashariki ya Kati.

Aidha, viongozi hao wawili walijadili mbinu za kuutatua mzozo wa mashariki mwa Ukraine wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa bunge siku ya Jumapili.