'Faiza agoma kurejea nchini kushuhudia ndoa ya Sugu'


Mwanadada asiyeishiwa na vijimambo mtandaoni, ambaye pia ni mzazi mwenzie na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu', FaizaAlly ambaye kwa sasa yupo nchini China kwa safari zake za kikazi, aja na hili jipya kuhusu taarifa za Sugu kufunga ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza amedai ameamua kughairi tarehe ya kurudi Tanzania kupisha ndoa ya mzazi mwenzie. Ameelezea hali atakayokuwa nayo huku akisema itamuuma kwani bado anampenda Sugu.

Kama hiyo haitoshi, Faiza pia amegoma kumtakia kheri mzazi mwenzie kwenye ndoa yake anayotarajia kufunga siku za hivi karibuni. Wawili hao kipindi cha mahusiano yao, walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Sasha.