Loading...

8/13/2019

Hili jambo tutalifikisha katika mamlaka za juu - David Kafulila


Na Baraka Messa- Songwe

Mnada wa kwanza zao la kahawa mikoa ya nyanda za juu kusini  mkoani Songwe msimu wa 2019 umevunjika kutokana na bodi ya kahawa kuonyesha dalili za kumhujumu mkulima na kwenda kinyume na agizo la serikali la kutaka sehemu zote ambazo zao la hilo kutaka kuwa na mnada ambao lengo likiwa ni kumnufaisha mkulima .

Hayo yameibuka leo (jana ) katika kikao cha bodi ya kahawa kilichoshirikisha, wakulima viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa zao hilo mkoani songwe.

Katibu tawala  Mkoa wa Songwe David Kafulila alisema kuwa mnada huo uliofanyika August 9 mwaka huu umefutwa kutokana na kuonekana kutokuwa na manufaa hata kidogo kwa wakulima wa zao la kahawa  kwa kukosa uwazi na kutoonyesha kama kuna mnada wa kahawa unaofanyika Songwe.

Baada ya hapo aliwaahidi wakulima kuwa wote waliohusika katika hujuma hizo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kutokana na hujuma walizozionyesha.

Alisema kutokana na ripoti ya wakulima walioitoa katika kikao hicho ilionyesha dhahiri kuwa bodi ya kahawa haipo kwa niaba ya kumnufaisha mkulima bali wapo kwa ajili ya kumnyonya na kuwatetea  na wanunuzi na madalali wa zao hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi wa mkoa wa Songwe.

“Hili jambo tutalifikisha katika mamlaka za juu ili hatua stahiki ziweze kufanyika kuna haja ya kuvunja bodi kutokana na hujuma za kumdhulumu mkulima wa zao la kahawa katika mikoa hii ya nyanda za juu kusini” alisema Kafulila.

Awali Charles Chenza Mwenyekiti wa kamati ndogo iliyoundwa na wakulima kufuatilia na kuchunguza mwenendo wa mnada wa kwanza kufanyika mkoani songwe baada ya serikali kuagiza mnada wa kahawa kufanyika kila kanda ambako zao hilo huzalishwa alisema kuwa wamegundua changamoto mbalimbali ambazo moja kwa moja zina mnyonya mkulima

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger