Hili ndio Taifa lisilo na uwakilishi wa wanawake bungeni


"Sio jambo la kawaida kuwa na viwango vya juu vya dhulma dhidi ya wanawake. Sio jambo la kawaida kwamba hatuna wanawake katika mchakato wa kubuni sheria", anasema Yasmin Bjornum, mwanaharakati wa kutetea usawa wa kijinsia nchini Vanuatu.

Bunge katika nchi yake ambayo imebuniwa kutokana na visiwa 80 ambavyo umbali wake ni kilomita 1,300 kusini mwa bahari ya Pacifiki ina jumla ya wabunge 52.

Cha kushangaza ni kuwa wabunge wote ni wanaume - hali inayoifanya kuwa moja ya nchi tatu duniani zilizo na wabunge wanaume pekee.

"Masuala yanayotuhusu hayaangaziwi katika asasi zote za juu nchini zinazofanya maamuzi ya nchi," anasema Bjornum.

Kukabiliana na hali hiyo mwaka 2016 alianzisha ukimbi wa Sistamatandaoni kwa lengo la kuwahamasisha wanawake wenzake juu ya haki zao, akiwa na matumaini baadhi yao wavutiwa na juhudi hizo na kuungana nae.

Wanawake wa Vanuatu wanaopania kujiunga siasa wanakabiliwa na vizuizi vya kila aina, hasa ikizingatiwa kuwa baraza la kitamaduni lina jukumu kubwa kuamua masuala ya kijamii katika nchi hiyo hususan katika maeneo ya vijijini ambako watu wengi wanaishi.

Mabaraza hayo yanaongozwa na wanaume wanaofahamika kama machifu, ambao pia wanapendekeza nani ateuliwe kuwania kiti cha ubunge.

"Vyama vyote vya kisiasa nchini (Vanatu) vinaongozwa na wanaume. wanateua wagombea ambao baadae wanachaguliwa bungeni.

Hatua hiyo imechangia wawakilishi wote bungeni kuwa wanaume,"anasema mbunge wa zamani Bi Hilda Lini.

Lini alikuwa mbunge wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa mwaka 1987  na alihudumu kwa miaka 11 katika mihula mitatu tofauti pia ni mmoja wa wanawake watano waliowahi kushikilia wadhifa huo nchini.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia