Huawei wazindua mfumo mpya HarmonyOS, waahidi kupindua soko la Android


Kampuni ya utengenezaji wa simu Huawei imezindua rasmi mfumo wake endeshi (Operating System) ujulikanao kwa jina la HarmonyOS utakaotumika kwenye simu zao za Huawei.

Akiongea kwenye mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Richard Yu amesema mfumo huo utakuwa wa spidi zaidi kwenye simu na Smart TV kuliko hata ule wa Android.

Yu amesema kuwa mfumo wa HarmonyOS ulianza kutengenezwa tangu mwaka 2017 ulijulikana kwa jina la HongmengOS kabla ya leo kuzinduliwa.

Mfumo wa HarmonyOS utaanza kutumika rasmi kwenye matoleo mapya ya Honor Series na kwa watumiaji wa simu za zamani zenye mfumo wa Android watachagua aidha waendelee kutumia Android au kubadilisha mfumo wa HarmonyOS.

Kiutendaji, mfumo huo utasapoti program zote zilizoandikwa kwa kutumia lugha ya kompyuta ya HTML5 pamoja na Linux.

Kwenye mkutano huo pia, Huawei wamesema kuwa lengo la mfumo wao mpya wa HarmonyOS ni kupindua soko la mfumo wa Android duniani, Huku wakiaminisha umma kuwa mfumo wao ni bora na ni salama zaidi.