Idadi ya waliofariki kwa ajali ya moto Morogoro yaongezeka


Majeruhi mmoja wa ajali ya moto mjini Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amefariki leo Ijumaa Agosti 23, 2019 kati ya majeruhi 15.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Muhimbili,  Aminiel Aligaesha amesema majeruhi 14  wapo chini ya uangalizi maalum.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 10, 2019, Msamvu barabara ya Morogoro-Dar es Salaam baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.

Tangu siku hiyo hadi Agosti 11, 2019 watu 100 waliripotiwa kufa huku wengine 15 wakiendelea na matibabu MNH na leo mmoja amefariki.




Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items